Njia ya kupata fedha kwa uhuru

Kupitia kuwa Afisa wa kampuni kubwa anayelipwa vizuri (Highly paid executive). Ukiwa mkurugenzi mkuu mtendaji wa TBL, CRDB, Cocacola, Vodacom etc mshahara wako ni milioni 20 au zaidi pamoja na marupurupu mengine ya kumwaga kila mwezi. Hivyo hawa mabosi tayari wana nafasi kubwa ya uhuru wa kifedha kama wataweka akiba na kuwekeza kwenye assets. Kama unavutiwa na njia hii jambo pekee ni kufanya bidii ya ‘kufufuka mtu and to ‘keep your nose clean’ throughout your career.
Na uwe tayari, sometime, kufanya kazi kwa miaka mingi sana ili kufika juu. Asilimia 10 ya matajiri wote duniani wanatoka kundi hili.
2. Kupitia kuwa mwanataaluma aliyebobea. Flying doctors, (Think about the Ben Carsons of this world), wanasheria wakuu, top accountants etc! Wanalipwa vizuri. Hapa inabidi uwe umeenda shule kweli kweli ili ufike huko. Kama hauko vizuri darasani, huwezi ku win kwa njia hii. 10% ya matajiri wote wanatoka hapa.
3. Watu wa mauzo au mameneja wa mauzo. Hawa hufika juu kama wako kwenye makampuni yenye kamisheni kwa wale wanaofanya vizuri! Huwa hakuna kikomo cha idadi ya watu unaoweza kuwauzia kama una ujuzi wa kutosha wa bidhaa unayoiuza, mipango mizuri inayotekelezeka na bidii ya hali ya juu. 5% ya matajiri wote hutokea kundi hili.
4. Watu wenye vipaji maalum; wanamichezo nyota, wanamuziki maarufu (The Diamonds of this world) wachekeshaji kama akina Masanja, Joti, nje akina Jerry Seinfeld, Chris Rock, Chris Tucker etc, waandishi mashuhuri akina John Grisham, Paolo Coelho, kina Shigongo hapa nyumbani n.k. Hawa huwa ni 1% tu ya matajiri wote ulimwenguni. Watu wengi hudhani hawa huwa ni wengi kwa sababu ya kufahamika kwao kupitia vyombo vya habari!
Sasa, guess what? Unajua tumebakisha asilimia ngapi?
74%. Yes 74%!. Asilimia 74 ya matajiri wote duniani ni WAJASIRIAMALI. Kuanzia kuuza mayai ya kanga, kufuga sungura, kuuza mazao, maduka, migahawa, elimu, internet biz, network marketing etc. Wote huo ni ujasiriamali. 
Watu wengi wana nafasi kubwa zaidi ya kufanikiwa kwenye ujasiriamali kuliko hayo maeneo mengine manne.
Ndiyo maana ninahubiri ujasiriamali! Najua ninaweza kuwasaidia watu wengi kupitia njia hii kuliko kupitia kuwa highly paid execs or professionals. But still jambo la muhimu sana kwako ni kufuata kitu ambacho roho yako inapenda.
Swali muhimu ni wewe unachagua mlango gani katika milango hii mitano?
Japo kuwa inawezekana kuwa na mlango zaidi ya mmoja, chagua kwanza mlango mmoja halafu fanya kweli yaani simama imara halafu mengine yanawezafuata!

Comments

Popular posts from this blog

MAANA YA DIVAI

NAMNA YAKUTENGENEZA SABUNI AINA ZOTE

UFUGAJI WA KUKU KWA UTAALAMU