Posts

Showing posts from November, 2014

fahamu Jinsi yakuweka hisa

Msingi na ustadi wa kuwekeza kwenye Soko la Hisa JE ukiwa kama mwananchi wa kawaida usingependelea kuwa mmiliki wa kampuni bila ya kuwa na ulazima wa kufika kazini na kufanya kazi za kila siku? Hebu tafakari kwa kina, upo nyumbani kwako umepumzika au ukifanya shughuli zako nyingine na ukiiangalia kampuni yako inakua kwa ufanisi na tija na baada ya muda unachukua hundi yako ya gawio huku mtaji wako ukiendelea kukua kila kukicha. Jambo hili linaweza kuonekana kama ni njozi au ndoto, lakini ukweli ni kwamba lina ukweli usiopingika na jawabu lake ni kuwa na hisa hususani katika kampuni zilizoorodheshwa katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE). Kwa hiyo ili kutimiza ndoto yako ya kukidhi mahitaji yako ya fedha na kuanza safari yako ya kumiliki kampuni kupitia Soko la Hisa unatakiwa kuwa na uelewa mzuri wa jinsi gani hisa zinavyouzwa na kununuliwa katika soko la hisa. Katika kipindi cha zaidi ya muongo mmoja uliopita, wananchi wengi wa kawaida nchini Tanzania wamekuwa na s

Faida za mti wa Mlonge

Image
UTANGULIZI Mti wa Mlonge una faida nyingi ambazo hazifahamiki kwa watu wengi. Faida za mti huu zinatokana na sehemu mbalimbali za mti huu ambazo ni maua, majani, magome na matunda na zina faida nyingi kwa afya ya binadamu. Maua ya mlonge huzalishwa hata kipindi ambacho hakuna mvua. Mti huu una viinilishe ambavyo huweza kutumika kuboresha afya ya watoto wakati wa njaa. Majani ya mti huu yanastawi hata kipindi cha ukame ambapo ukuaji wa mazao ya chakula ni mdogo. Majani haya yana kiwango kikubwa cha vitamin B na C. Tafiti mbalimbali zilizofanyika zimeonyesha kuwa Mlonge una faida zifuatazo: • Unaongeza kinga ya mwili • Majimaji ya majani hutumika kama dawa ya     ngozi • Majimaji ya majani hurekebisha msukumo wa damu • Unapunguza maumivu ya kichwa • Majimaji ya majani yanatumika kurekebisha kiwango cha sukari mwilini hasa kwa watu wenye          tatizo la kisukari • Unapunguza uvimbe na maumivu ya viungo • Unaongeza kiwango cha maziwa kwa akina mama wanaonyonyesh