Posts

Showing posts from April, 2016

UZALISHAJI WA TIKITI MAJI (WATER MELON)

KILIMO CHA TIKITI MAJI Utangulizi Matikiti maji hulimwa kama zao la biashara katika sehemu nyingi duniani zenye hali ya hewa ya joto la wastani. Zao hili lina wapatia watu shughuli za kufanya na hivyo kuwapatia kipato kuanzia kwenye nyanja za uzalishaji hadi kwenye matumizi. Matikiti maji ni mojawapo ya jamii aina ya matunda au mbogaboga inayotambaa. Mimea hii inapatikana katika kundi linalojumuisha mimea mingine kama kama matango,maboga na maskwash. Zao la tikiti maji ni mojawapo ya zao ambalo lina faida kubwa sana ukilinganisha na mazao mengine kwa muda mfupi. Katika shamba la ukubwa wa shamba la ekali moja(1.acre) lililoandaliwa vizuri, kupandwa na kuhudumiwa vizuri mkulima ana uwezo wa kuvuna kiasi cha TANI 15-36, ambacho kitamsaidia kupata fedha zitakazo msaidia katika mahitaji yake mbalimbali na kuondokana na Umasikini. Tikiti maji ni moja ya mazao ya matunda ambayo yamejipatia umaarufu mkubwa kote ulimwenguni. Zao ili ni moja ya mazao ambayo ni rahisi sana kuzalisha na lisiloh

UFUGAJI WA KUKU (KUZINGATIA)

Image
Wafugaji wengi wa Tanzania wanafuga kuku wa kienyeji. Ndege hawa kwa kawaida wanafugwa sehemu za vijijini ambapo wanaachiwa huru kuzurura. Kuna uwezekano mkubwa sana wa kizazi kujirudia kwa kuwa jogoo anaweza kumpanda mtetea ambaye alitokana naye, au kumpanda mtetea ambaye wamezaliwa pamoja. Kuzaliana kwa namna hiyo kunasababisha matatizo makubwa, ikiwa ni pamoja na kudumaa, kupunguza uzalishaji wa mayai, kuwa na vifaranga dhaifu ambavyo ni rahisi kushambuliwa na magonjwa, na mengineyo mengi yasiyokuwa ya kawaida. Ufugaji huru ambao una udhibiti ni muhimu sana ili kuepuka kizazi kujirudia. Kuku wanaweza kuwekwa kwenye makundi na kuachiwa kwa makundi ili kuzuia uwezekano wa kuzaliana kwa kizazi kimoja. Mfugaji anayetaka kufanikiwa katika ufugaji wa kuku wa kienyeji ni lazima achanganye mbinu za kienyeji na za kisasa. Hii inajumuisha njia zifuatazo: Kuchagua aina/mbegu Kuchagua mbegu inamaanisha: Mtetea au jogoo mwenye ubora wa hali ya juu , akiwa na sifa kama uzalish

Elimu ununuzi wa hisa

Image
Wapewa elimu ununuzi wa hisa  Kuchapa     Barua pepe Dk Charles Kimei, Mkurugenzi Mkuu wa CRDB. WANAHISA wa benki ya CRDB tawi la Shinyanga mjini wamepatiwa elimu zinazohusu masuala ya ununuzi wa hisa ili wanufaike na fedha zao. Elimu hiyo imepongezwa na wanachama hao ambao walikuwa na mengi ya kutaka kujua kuhusu uwekezaji na benki yao. Wanachama hao Deogratius Sulla na Amani Mkulo, kwa nyakati tofauti waliipongeza benki hiyo kwa kutambua umuhimu wao ambapo wamewapatia elimu ambayo hawakuwa nayo juu ya kununua hisa. Awali akitoa elimu hiyo ya ununuzi wa hisa Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga mjini, Saidi Pamui aliwashauri wanachama hao kuwa makini katika mauzo na ununuzi wa hisa. “Unapotaka kununua hisa kwenye kampuni yoyote ile kitu cha kwanza cha kufanya unatakiwa uangalie afya ya kampuni na siyo kukurupuka au kutafuta ushauri kwa wataalamu,” alisema Pamui. Naye Meneja wa Idara ya Kilimo na Biashara kutoka benki hiyo makao makuu jijini Dar e