FAIDA YA TANGAWIZI (GINGER)

Bookmark and Share
Tangawizi (Ginger):
tangawiziTangawizi ni nini?
Tangawizi ni kiungo ambacho kinatokana na mizizi ya mmea wa Tangawizi. Mmea huu unafanana sana na Binzari ikiwa bado haijamenywa maganda yake. Na kwa hapa Tanzania Tangawizi hulimwa sana mikoa ya nyanda za juu Kusini na baadhi ya mikoa kama Kilimanjaro, baadhi ya maeneo ya mkoa wa Manyara, Morogoro, na kwingineko nchini.
Pia kama bidhaa inapatikana nchi nzima kwa bei nafuu kabisa na kila mtu mwenye uwezo wowote wa kiuchumi anaweza kununua aidha kwa kipande kimoja, fungu au kwa kilo pia.
Tangawizi inatumikaje?:
Mmea huu unaweza kuonekana kama mmea wa kawaida na watu kuutumia tu kama mazoea lakini Kiungo hiki kinaweza kutumiwa kama Dawa. Kiungo hiki huweza kutumika kikiwa kibichi au kikiwa kimekaushwa na kutengenezwa unga.
Nini Faida ya Tangawizi?
Tangawizi ni mmea kati ya mimea mingi yenye maajabu, Mmea huu unaweza kutumika kama dawa na kutibu magonjwa mengi tu zaidi ya 72 yaliyo ndani ya miili yetu na kutuacha tukiwa wazima na kutekeleza majukumu yetu ya kila siku.
Pia kiungo hiki kinafaida zaidi kwa Wagonjwa hasa walio athirika na Ugonjwa wa UKIMWI. Hivyo chonde kwa wale wenye matatizo kama haya wanaweza kupata faida zaidi ya Maajabu ya Mmea huu wa Tangawizi.
Jinsi ya kuitumia kama Dawa:
Tangawizi ikiwa imesagwa au Mbichi iliyopondwa pondwa inaweza kutumika kama Kinywaji kama ilivyozoeleka kwa watu wengi. Namna rahisi ya kuitumia Tangawizi ni katika chai, inakuwa ni mubadala wako wa majani yale meusi ya chai ambayo yenyewe huwa na kaffeina ambayo hupelekea magonjwa mengi mwilini(soma kuhusu kansa na uzito kupita kiasi kuyajuwa madhara ya kutumia majani ya chai nyeusi), Pia inaweza kutumika katika vyakula hasa nyama na mbogamboga zingine, inaweza kuongezwa katia juisi freshi pia na kuleta radha nzuri ambayo ni dawa pia.
Hutibu Magonjwa gani?
Tangawizi husaidia yafuatayo:
  • Kuongeza hamu ya kula
  • Kupunguza kichefuchefu
  • Kutapika, kuharisha
  • Kisukari
  • Shinikizo la damu
  • Kuongeza msukumo wa damu
  • Kutoa sumu mwilini
  • Maumivu ya tumbo na
  • Gesi tumboni.
Pia husaidia uyeyushwaji wa chakula tumboni. Vilevile husaidia wakati wa matatizo ya mafua au flu na magonjwa mengine mengi.
tangawizi 1Kama utakuwa makini au kuwahi kuwahudumia wagonjwa wa UKIMWI basi magonjwa hayo hapo juu ni kati ya Magonjwa nyemelezi yanao wasumbua sana hawa ndugu zetu hivyo wakitumia Tangawizi basi wataweza kuondokana kabisa na matatizo hayo na kuishi vizuri na kutekeleza majukumu yao ya kila siku na kuepukana na kulala tu kitandani.



Comments

Popular posts from this blog

MAANA YA DIVAI

NAMNA YAKUTENGENEZA SABUNI AINA ZOTE

UFUGAJI WA KUKU KWA UTAALAMU