NJIA YA KUWA MJASIRIAMALI BORA

1. MAWASILIANO NA WAJASIRIAMALI WENGINE Jenga urafiki nao kuwa karibu nao mara kwa mara maana mnafanana katika biashara, toka nao kwenda sehemu mbali mbali ili uweze kujifunza mengi kutoka kwao. 2. DAIMA JIAMINI Amini kuwa kile unachokifanya kipo sahihi na sio kama una bahatisha 3. MATANGAZO NA SOKO Tangaza biashara yako ili uweze kupata wateja wengi zaidi na kuweza kujulikana haraka, soko linakuja kama utakuwa unafahamika. 4. KUTAFUTA NJIA RAHISI Usitumie pesa nyingi sana maana biashara yako ndio kwanza inaanza kwa hiyo unahitajika kuangalia njia rahisi ya kuweza kubana matumizi yako. 5. KUUNGANA NA WAJASIRIAMALI WENGINE KUPITIA MITANDAO YA KIJAMII Kuna mitandao mingi ya kijamii kama vile Facebook, Twitter, My Space n.k ni vema kuitumia hii kama kiunganishi kikubwa na wajasiriamali wengine na wateja ili kuweza kuongeza maendeleo. 6. KUTENGENEZA WEBSITE YAKO Kuwa na site yako binafsi ni nzuri maana itasaidia kufanya kazi kwa urahisi na kisasa kabisa, fungua website yako na uweke bidhaa zako ili uweze kuwavutia wateja wako. 7. KUJIFUNZA MAKOSA Angalia pale ulipokosa na ujifunze usije kurudia tena lile kosa la mwanzo. 8. KUFANYA KIPAJI CHAKO KAMA KAZI YAKO Chukulia unachokifanya ni kama kazi yako yani kama vile waziri anavyotoka kwake na kwenda Wizarani kazini. 9. KUHUDHURIA SEMINA Kuhudhuria semina mbali mbali za mafunzo ya ujasiriamali ili kupata knowledge zaidi. 10. TAFUTA MBINU RAHISI YA KUTATUA TATIZO KUBWA Siku zote ona tatizo kubwa kama la kawaida sana na usipanic ona ni jambo rahisi sana usijijengee kushindwa.

Comments

Popular posts from this blog

MAANA YA DIVAI

NAMNA YAKUTENGENEZA SABUNI AINA ZOTE

UFUGAJI WA KUKU KWA UTAALAMU