UTAFITI uliofanywa nchini Marekani hivi karibuni unaonesha kuwa katika miaka ya 1950, wastani wa ulaji wa mayai ya kuku ulikuwa mayai 375 kwa mtu mmoja, lakini hadi kufikia mwaka 2007, kiwango hicho kimepungua hadi kufikia mayai 250 tu kwa mtu mmoja, ikiwa ni punguzo la asilimia 33. Sababu moja wapo ya kushuka kwa ulaji wa mayai imeelezwa kuwa, pamoja na sababu zingine, ni imani potofu kwamba mayai husababisha ugonjwa wa moyo na kwa wagonjwa wa moyo hawaruhusiwi kabisa kula mayai kwa madai kwamba yana kiwango kikubwa cha kolestro. Hata hivyo, tafiti kadhaa zilizofanyika kuhusiana na imani hiyo potofu zimeonesha HAKUNA uhusiano wowote kati ya kuongezeka kolestro mwilini na ulaji wa mayai na kwamba mayai HAYASABABISHI ugonjwa wa moyo, iwapo mayai hayo ni halisi. Katika siku za karibuni, tumeshuhudia kuibuka kwa ufugaji wa kuku kwa kiwango cha hali ya juu, ambapo kuku hufugwa kwa kulishwa vyakula na madawa maalum yanayowawezesha kukua ndani ya muda mfupi au kutoa mayai mengi. Ha...
HISA NI NINI? Hisa ni mgao (share) ya umiliki wa kampuni au biashara yoyote kubwa. Unaponunua hisa maana yake umetoa fedha kwa ajili ya uendeshaji wa kampuni au biashara husika kwa hiyo na wewe ni miongoni mwa wamiliki na nguvu au umuhimu wako unatokana na mgao ulionao. Kama kampuni ina mtaji wa shilingi laki moja na wewe umenunua hisa za shilingi elfu hamsini, maana yake utakuwa na nguvu ya kushiriki hata kwenye maamuzi nyeti yahusuyo kampuni au biashara husika, tofauti na mtu mwenye hisa za kwa mfano shilini elfu kumi. Soko la hisa (stock exchange) ni mfumo wa kibiashara ambapo wajasiriamali na wafanyabiashara, hununua vipande (stock) za kampuni au biashara na kuwekeza fedha zao kwenye mtaji kwa lengo la kuisaidia biashara husika kuendelea kukua. Soko kubwa zaidi duniani lipo jijini New York, Marekani likiwa na jina la New York Stock Exchange (NYSE). Kwa mujibu wa shirika la fedha duniani, soko la hisa ndiyo linaloongoza kwa kuingiza fedha nyingi kwenye mzunguko kuliko biashara nying...
SOMO LA KWANZA : UTENGENEZAJI WA SABUNI ZA AINA ZOTE. MASOMO YATAKAYO FUNDISHWA HAPA NI : 1 1. Utengenezaji Wa Sabuni isiyo na garama. 22. Utengenezaji Wa Sabuni ya urembo. 33. Utengenezaji Wa Sabuni ya asali na cream. 4 4. Utengenezaji Wa Sabuni ya manukato. 5 5. Utengenezaji Wa Sabuni ngumu. 66. Utengenezaji Wa Sabuni ya unga 77. Utengenezaji Wa Sabuni ya kugandisha. 8 8. Utengenezaji Wa Sabuni za dawa. 99. Utengenezaji Wa Sabuni za rangi. 110. Utengenezaji Wa Cream ya kunyolea. 111. Utengenezaji Wa Sabuni iliyotengenezwa na mafuta mengine. VIFAA VYA UTENGENEZAJI SABUNI. *Sufuria. *Bakuli kubwa la mfinyanzi au plastiki. *Mafuta *Maji. *Sodium hydroxide{NaOH} *Ubao mdogo/mw...
Comments
Post a Comment