Faida za mti wa Mlonge
UTANGULIZI Mti wa Mlonge una faida nyingi ambazo hazifahamiki kwa watu wengi. Faida za mti huu zinatokana na sehemu mbalimbali za mti huu ambazo ni maua, majani, magome na matunda na zina faida nyingi kwa afya ya binadamu. Maua ya mlonge huzalishwa hata kipindi ambacho hakuna mvua. Mti huu una viinilishe ambavyo huweza kutumika kuboresha afya ya watoto wakati wa njaa. Majani ya mti huu yanastawi hata kipindi cha ukame ambapo ukuaji wa mazao ya chakula ni mdogo. Majani haya yana kiwango kikubwa cha vitamin B na C. Tafiti mbalimbali zilizofanyika zimeonyesha kuwa Mlonge una faida zifuatazo: • Unaongeza kinga ya mwili • Majimaji ya majani hutumika kama dawa ya ngozi • Majimaji ya majani hurekebisha msukumo wa damu • Unapunguza maumivu ya kichwa • Majimaji ya majani yanatumika kurekebisha kiwango cha sukari mwilini hasa kwa watu wenye tatizo la kisukari • Unapunguza uvimbe na maumivu ya viungo • Unaongeza kiwango cha m...
Comments
Post a Comment