NJIA ZA KUFIKIA MALENGO KATIKA MAISHA
KATIKA sayansi ya mafanikio kuna mambo mengi sana yanahusika kutufikisha pale tunapopataka. Pia kuna njia tofauti zinazopendekezwa na wataalamu wa masuala ya saikolojia. Mfano mwanafilosofia wa Ugiriki, Aristotle anasema: “Binadamu ni kiumbe wa malengo.” Pia kuna watu wanaweza wakahoji kwa nini tuwe na malengo katika maisha yetu ya kila siku. Zifuatazo ni sababu chache tu za kwanini tuwe na malengo. Kwa sababu mafanikio ni malengo na vingine vinafuata kwa hiyo kama unataka mafanikio ya kweli inabidi uwe na malengo, bila malengo unakuwa ni sawa na kisiwa chenye utajiri mwingi, lakini bado hakijavumbuliwa, kwa hiyo jitahidi uwe na malengo ikiwa ndiyo njia ya kufanikiwa. Malengo ni kama mafuta katika safari ya kufanikiwa, umuhimu wa malengo unafananishwa na mafuta katika gari kwani bila mafuta haiwezi kwenda, ni sawa na malengo katika kazi hata kama una bidii sana kufanya kazi bila malengo itakuwa vigumu kupima utendaji wako mwenyewe wa kazi wa kila siku. Malengo yanakusaidia kufikir...