NJIA YA KUWA MJASIRIAMALI BORA
1. MAWASILIANO NA WAJASIRIAMALI WENGINE
Jenga urafiki nao kuwa karibu nao mara kwa mara maana mnafanana katika biashara, toka nao kwenda sehemu mbali mbali ili uweze kujifunza mengi kutoka kwao.
2. DAIMA JIAMINI
Amini kuwa kile unachokifanya kipo sahihi na sio kama una bahatisha
3. MATANGAZO NA SOKO
Tangaza biashara yako ili uweze kupata wateja wengi zaidi na kuweza kujulikana haraka, soko linakuja kama utakuwa unafahamika.
4. KUTAFUTA NJIA RAHISI
Usitumie pesa nyingi sana maana biashara yako ndio kwanza inaanza kwa hiyo unahitajika kuangalia njia rahisi ya kuweza kubana matumizi yako.
5. KUUNGANA NA WAJASIRIAMALI WENGINE KUPITIA MITANDAO YA KIJAMII
Kuna mitandao mingi ya kijamii kama vile Facebook, Twitter, My Space n.k ni vema kuitumia hii kama kiunganishi kikubwa na wajasiriamali wengine na wateja ili kuweza kuongeza maendeleo.
6. KUTENGENEZA WEBSITE YAKO
Kuwa na site yako binafsi ni nzuri maana itasaidia kufanya kazi kwa urahisi na kisasa kabisa, fungua website yako na uweke bidhaa zako ili uweze kuwavutia wateja wako.
7. KUJIFUNZA MAKOSA
Angalia pale ulipokosa na ujifunze usije kurudia tena lile kosa la mwanzo.
8. KUFANYA KIPAJI CHAKO KAMA KAZI YAKO
Chukulia unachokifanya ni kama kazi yako yani kama vile waziri anavyotoka kwake na kwenda Wizarani kazini.
9. KUHUDHURIA SEMINA
Kuhudhuria semina mbali mbali za mafunzo ya ujasiriamali ili kupata knowledge zaidi.
10. TAFUTA MBINU RAHISI YA KUTATUA TATIZO KUBWA
Siku zote ona tatizo kubwa kama la kawaida sana na usipanic ona ni jambo rahisi sana usijijengee kushindwa.
Comments
Post a Comment