FAHAMU HISA NI NINI
HISA NI NINI?
Hisa ni mgao (share) ya umiliki wa kampuni au biashara yoyote kubwa. Unaponunua hisa maana yake umetoa fedha kwa ajili ya uendeshaji wa kampuni au biashara husika kwa hiyo na wewe ni miongoni mwa wamiliki na nguvu au umuhimu wako unatokana na mgao ulionao.
Kama kampuni ina mtaji wa shilingi laki moja na wewe umenunua hisa za shilingi elfu hamsini, maana yake utakuwa na nguvu ya kushiriki hata kwenye maamuzi nyeti yahusuyo kampuni au biashara husika, tofauti na mtu mwenye hisa za kwa mfano shilini elfu kumi.
Soko la hisa (stock exchange) ni mfumo wa kibiashara ambapo wajasiriamali na wafanyabiashara, hununua vipande (stock) za kampuni au biashara na kuwekeza fedha zao kwenye mtaji kwa lengo la kuisaidia biashara husika kuendelea kukua. Soko kubwa zaidi duniani lipo jijini New York, Marekani likiwa na jina la New York Stock Exchange (NYSE).
Kwa mujibu wa shirika la fedha duniani, soko la hisa ndiyo linaloongoza kwa kuingiza fedha nyingi kwenye mzunguko kuliko biashara nyingine zozote, takwimu zinaonesha kuwa mwaka 2008, mtaji katika soko la hisa dunia nzima ulikuwa ni dola za Kimarekani, trilioni 36.6 na mpaka mwezi Juni mwaka huu, mtaji ulikuwa umepaa na kufikia dola za Kimarekani trilioni 791, ikiwa ni mara kumi na moja zaidi ya uchumi wa dunia.
Huu ni uthibitisho kuwa soko la hisa linakua kwa kasi kubwa na ndiyo lililoushikilia uchumi wa dunia. Kwa msingi huo, ni lazima kila mjasiriamali ajifunze juu ya soko la hisa ili kuyafikia mafanikio ya kweli.
Tunashukuru sana kwa maelezo mafupi lakini yenye kueleweka. Tutashukuru sana kama utarudi tena na maelezo ya kina juu ya somo hili la hisa ili kutufungua mawazo zaaidi sisi watanzania
ReplyDelete