Faida za pilipili kiafya
Japokuwa Pili pili inaliwa na watu wa jamii mbali mbali, Faida na Afya ya kula pilipili wengi hawazijui au hazijulikani na watu wengi.
Kwenye pilipili kuna kemikali iitwayo Capsaicin, ambayo ndio inayo sababisha muwasho na joto la pilipili.
Pilipili inasaidia sana kusawazisha sukari kwenye damu
Ulaji wa pilipili kunaweza kunawasaidia sana watu wanene (overweight) au wanao ugua ugonjwa wa kisukari. Hii ni kwa mujibu wa timu ya watafiti katika Chuo Kikuu cha Tasmania, utafiti iliyochapishwa katika American Journal of Clinical Nutrition, mwezi Julai 2006.
Utafiti huo pia umeonyesha kwamba kawaida ya kula Pilipili kunaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa kudhibiti na kusawazisha insulini kwa 60%. baada ya kula chakula.
Pilipili husaidia kupunguza maumizi na uvimbe kwenye tezi na vilevile huwasaidia wagonjwa wa rheumatoid na arthritis kupata nafuu. Vile vile husaidia kuondoa mkusanyiko wa damu sehemu moja ya mwili
Pilipili usaidia kufungua kwa haraka na kwa ufanisi pua zilizoziba kwa mafua, kuruhusu kupumua kwa urahisi zaidi!
Pilipili pia husaidia kupunguza upatikanaji wa saratani ya kwenye tumbo (Stomach Cancer)
Pilipili usaidia kuongezeka kwa kiwango cha metabolic, ambayo husaidia kuchoma mafuta, ulaji wa pilipili kunaweza kuinua kiwango na metabolic yako hadi 23% ndani ya masaa 3.
Kula pilipili usaidia kupunguza cholesterol, na kupunguza kiasi cha fibrin katika damu.
Comments
Post a Comment