JINSI YAKUTENGENEZA MANGO PICKLES
UTENGENEZAJI WA MANGO PICKLES
Mango Pickles |
MANGO PICKLES au " ACHARI YA EMBE " ni chachandu inayo tumika kunogesha utamu wa chakula. Malighafi kuu katika utengenezaji wa " MANGO PICKLES " ni embe.
MATAYARISHO
* Embe zisafishwe vizuri kwa kuosha vizuri kwa kutumia maji masafi.
( Embe zioshwe kabla hazijamenywa )
* Embe likatwe katwe vipande bila kuligusa kokwa, vipande hivyo viwekwe kwenye kichanja baada ya kukatwa katwa na vianikwe juani kwa muda wa nusu saa.
* Hifadhi embe zako hizo kwenye chombo kisafi, kwa muda wa siku tano.
KUTENGENEZA MANGO PICKLES
* Tayarisha nyanya robo kilo, menya maganda na katakata vipande vidogo.
* Katakata vitunguu viwili vikubwa.
* Chumvi vijiko viwili vya chai.
* Vinegar _ kijiko kimoja cha chai kwa ajili ya kuifanya mango pickle yako isiharibike.
* Maji ya limao vijiko viwili vya chai.
Tengeneza rosti ya mchanganyiko wa malighafi zote zilizo tajwa hapo juu. Baada ya kutengeneza rosti hiyo, chukua vipand vyako vya embe na changanya na rosti yako.
Weka vipande vyako vya embe ndani ya rosti hii, kisha hifadhi katika kifungashio kwa ajili ya matumizi ..
N.B: Kwa kiwango hiki cha rosti una shauriwa uweke vipande vya embe vyenye uzito wa kilo moja.
Comments
Post a Comment