UFUGAJI WA KUKU KWA UTAALAMU
Mfugaji ili uwape kuku wako lishe bora yenye kuendelea, na ili upate matokeo bora zaidi katika ufugaji wako wa kuku basi yakupasa kuzingatia yafuatayo:- Tumia chakula bora na siyo bora chakula. Tumia chakula bora ambacho hakina madhara kwa kuku wako na hata walaji kwa ujumla. Weka chakula mahali safi na salama kuepuka wadudu waharibifu kama vile panya ili kuzuia maambukizi ya magonjwa kwa kuku. Tumia kanuni ya " least cost combination " yaan tumia chakula cha bei nafuu kinachotoa matokeo bora zaidi ili kupunguza gharama za ufugaji hali ambayo itakufanya upate faida mara dufu. Kwa kufanya hivyo utaweza kuwalisha kuku wako chakula kilicho bora kwa matokeo bora zaidi bila kuyumba kiuchumi wakati wote wa ufugaji wako. KUTUNZA KUMBUKUMBU KATIKA UFUGAJI Kuna usemi usemao " mali bila daftari hupotea bila habari " ukiwa na mradi wowote wa ufugaji ni vema ukiwa unaweka kumbukumbu za kila siku au kwa kila wiki. Katika kutunza kumbukumbu za ufugaji kun...