Elimu ununuzi wa hisa

Wapewa elimu ununuzi wa hisa


WANAHISA wa benki ya CRDB tawi la Shinyanga mjini wamepatiwa elimu zinazohusu masuala ya ununuzi wa hisa ili wanufaike na fedha zao. Elimu hiyo imepongezwa na wanachama hao ambao walikuwa na mengi ya kutaka kujua kuhusu uwekezaji na benki yao.
Wanachama hao Deogratius Sulla na Amani Mkulo, kwa nyakati tofauti waliipongeza benki hiyo kwa kutambua umuhimu wao ambapo wamewapatia elimu ambayo hawakuwa nayo juu ya kununua hisa.
Awali akitoa elimu hiyo ya ununuzi wa hisa Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga mjini, Saidi Pamui aliwashauri wanachama hao kuwa makini katika mauzo na ununuzi wa hisa.
“Unapotaka kununua hisa kwenye kampuni yoyote ile kitu cha kwanza cha kufanya unatakiwa uangalie afya ya kampuni na siyo kukurupuka au kutafuta ushauri kwa wataalamu,” alisema Pamui.
Naye Meneja wa Idara ya Kilimo na Biashara kutoka benki hiyo makao makuu jijini Dar es Salaam Maregesi Shabani, akitoa elimu kwenye semina hiyo aliwataka wanahisa hao kufungua akaunti ya Busara kwenye benki hiyo ambayo itawasaidia kupata gawio lao la hisa kwa uharaka kuliko kuandika hundi kupitia Posta.

Comments

Popular posts from this blog

Faida za mti wa Mlonge

MAANA YA DIVAI

NAMNA YAKUTENGENEZA SABUNI AINA ZOTE