UTAFITI uliofanywa nchini Marekani hivi karibuni unaonesha kuwa katika miaka ya 1950, wastani wa ulaji wa mayai ya kuku ulikuwa mayai 375 kwa mtu mmoja, lakini hadi kufikia mwaka 2007, kiwango hicho kimepungua hadi kufikia mayai 250 tu kwa mtu mmoja, ikiwa ni punguzo la asilimia 33. Sababu moja wapo ya kushuka kwa ulaji wa mayai imeelezwa kuwa, pamoja na sababu zingine, ni imani potofu kwamba mayai husababisha ugonjwa wa moyo na kwa wagonjwa wa moyo hawaruhusiwi kabisa kula mayai kwa madai kwamba yana kiwango kikubwa cha kolestro. Hata hivyo, tafiti kadhaa zilizofanyika kuhusiana na imani hiyo potofu zimeonesha HAKUNA uhusiano wowote kati ya kuongezeka kolestro mwilini na ulaji wa mayai na kwamba mayai HAYASABABISHI ugonjwa wa moyo, iwapo mayai hayo ni halisi. Katika siku za karibuni, tumeshuhudia kuibuka kwa ufugaji wa kuku kwa kiwango cha hali ya juu, ambapo kuku hufugwa kwa kulishwa vyakula na madawa maalum yanayowawezesha kukua ndani ya muda mfupi au kutoa mayai mengi. Ha...
Comments
Post a Comment