fahamu Jinsi yakuweka hisa
Msingi na ustadi wa kuwekeza kwenye Soko la Hisa JE ukiwa kama mwananchi wa kawaida usingependelea kuwa mmiliki wa kampuni bila ya kuwa na ulazima wa kufika kazini na kufanya kazi za kila siku? Hebu tafakari kwa kina, upo nyumbani kwako umepumzika au ukifanya shughuli zako nyingine na ukiiangalia kampuni yako inakua kwa ufanisi na tija na baada ya muda unachukua hundi yako ya gawio huku mtaji wako ukiendelea kukua kila kukicha. Jambo hili linaweza kuonekana kama ni njozi au ndoto, lakini ukweli ni kwamba lina ukweli usiopingika na jawabu lake ni kuwa na hisa hususani katika kampuni zilizoorodheshwa katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE). Kwa hiyo ili kutimiza ndoto yako ya kukidhi mahitaji yako ya fedha na kuanza safari yako ya kumiliki kampuni kupitia Soko la Hisa unatakiwa kuwa na uelewa mzuri wa jinsi gani hisa zinavyouzwa na kununuliwa katika soko la hisa. Katika kipindi cha zaidi ya muongo mmoja uliopita, wananchi wengi wa kawaida nchini Tanzania wamekuwa na s...